Ledama Ole Kina: Ongeza Malipo Ya Watumishi Wa Umma’ Kabla Ya Kukata Asilimia 3
Seneta wa Narok Ledama ole Kina amemkashifu Rais William Ruto kwa kutangaza mpango mpya ambao utawafanya wafanyikazi kuchangia asilimia tatu ya mishahara yao kwenye Hazina ya Makazi inayoendeshwa na serikali.
Katika taarifa leo Jumatatu,ole Kina ametoa maoni kinzani kwa serikali kwanza kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa angalau asilimia 10 kabla ya kutekeleza pendekezo hilo.
Jana Jumapili, Rais Ruto alitangaza kwamba kila Kenya itahitajika kuchangia angalau asilimia tatu ya mshahara wake kwa Hazina ya Makazi.
Rais Ruto alisema kuwa makato hayo yatasaidia Wakenya kupata nyumba za bei nafuu kupitia Hazina ya Makazi.
Ruto, ambaye hakutaja ni lini makato hayo yataanza kutekelezwa alisema kuwa serikali itakuwa ya kwanza kutekeleza mpango wa Hazina ya Nyumba kwa zaidi ya watumishi elfu mia 700,000 wa umma.
Kulingana na Rais, serikali itajenga zaidi ya nyumba 200,000 za bei nafuu kufikia 2027, huku tayari elfu 10,000 zikiwa zimejengwa Nairobi.