Home » Waziri Mutua: Kenya Yapanga Kuwahamisha Zaidi Ya Raia 300 Kutoka Sudan

Waziri Mutua: Kenya Yapanga Kuwahamisha Zaidi Ya Raia 300 Kutoka Sudan

Kenya imewahamisha wanafunzi 29 waliokuwa wamekwama nchini Sudan kutokana na mapigano kati ya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na jeshi.

 

Waziri wa Masuala ya Kigeni Alfred Mutua amesema leo hii Jumatatu kwamba wanafunzi hao walipitia Ethiopia ambapo wamesafiri kwa ndege hadi Addis Ababa kutoka Gondor na kisha Nairobi.

 

Katika taarifa hiyo hiyo, Mutua amesema kuwa ndege ya Kenya Airforce ilikuwa katika hali ya kusubiri ili kuwahamisha kundi la wanafunzi 18 waliokuwa wakisafiri kwa barabara kuelekea mpaka wa Sudan Kusini.

 

Kulingana na Mutua, kundi lingine kubwa la Wakenya katika ratiba iliyopangwa litasafirishwa kwa ndege mbili kutoka Port Sudan hadi Jeddah, na kisha watasafiri hadi Nairobi kwa Shirika la Ndege la Kenya (KQ).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!