Home » Koome Awaomba Radhi Wanahabari Kwa Kuvamiwa Na Polisi

Koome Awaomba Radhi Wanahabari Kwa Kuvamiwa Na Polisi

Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome amewaomba radhi wanahabari kufuatia tukio ambapo polisi waliwashambulia wanahabari wakati wa maandamano yalioitishwa na  Kiongozi wa Azimio Raila odinga wiki iliyopita.

 

Koome ameweka wazi kuwa uchunguzi kamili kuhusiana na tukio hilo  tayari  umeanzishwa dhidi ya  afisa wa polisi aliyeonekana kwenye video akivunja vioo vya gari moja na kufyatua ndani vitoza machozi.

 

 

Koome amesema iwapo afisa huyo pamoja na wengine watapatikana na hatia ya kukiuka sheria, atachukuliwa hatua za kisheria.

 

 

Kando na kuwaomba msamaha, mkuu huyo wa polisi aliwahakikishia wanahabari kuwa katika uongozi wake, atahakikisha kuna uhusiano bora baina ya polisi na waandishi wa habari.

 

 

“Nataka kuwahakikishia marafiki zetu kutoka kwa vyombo vya habari kwamba mashambulizi hayakuelekezwa kwao kwa makusudi. Tutaendelea kufanya kazi nanyi kwa karibu tunapopanga kuwajumuisha katika baadhi ya operesheni zetu zijazo,” alisema.

 

Koome alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano ya maafisa 12 wa polisi walioteuliwa kwa nafasi ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi katika Shule ya mafunzo ya Serikali ya Kenya.

 

 

Pia amefichua kupokea taarifa za kujeruhiwa kwa baadhi ya waandishi wa habari wakati wakiripoti maandamano hayo.

 

 

“Tumepokea malalamiko hayo na yanashughulikiwa tuvumilie na tupeni muda,” alisema.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!