Home » Mwili Wa Geoffrey ‘Jeff’ Mwathi Wafanyiwa Uchunguzi

Mwili Wa Geoffrey ‘Jeff’ Mwathi Wafanyiwa Uchunguzi

Makachero kutoka idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamekusanya sampuli zaidi kwa uchunguzi baada ya kuufukua mwili wa marehemu Geoffrey ‘Jeff’ Mwathi ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

 

Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali Johansen Oduor, aliyefanya uchunguzi wa pili baada ya mwili huo kufukuliwa huko Njoro, Kaunti ya Nakuru, amefichua kuwa sampuli zilichukuliwa ili kubaini ikiwa Mwathi alilawitiwa au la.

 

Maafisa wa upelelezi pia wamepima upana wa kifua cha Mwathi ili kubaini ikiwa aliruka kutoka kwenye ghorofa kupitia dirishani kama ilivyodaiwa wakati wa uchunguzi wa awali.

 

Dkt Oduor ameendelea kufichua kuwa uchunguzi wa pili wa maiti uliofanyika leo hii Ijumaa haukufichua tofauti zozote na wa kwanza, akiongeza kuwa Mwathi alifariki kwa majeraha mabaya kichwani.

 

Mabaki ya Mwathi yamezikwa tena muda mfupi baada ya uchunguzi wa pili huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha kifo hicho.

 

Kulingana na Dkt..Oduor ameomba muda zaidi akieleza kuwa ni vigumu kubaini chanzo hasa cha kifo bila uchanganuzi ufaao kwani mwili huo ulikuwa tayari umeoza.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!