Naibu Rais Rigathi Gachagua Apinga Uwezekano Wa Handsheki
Naibu wa rais Rigathi Gachagua amesisitizi serikali ya William ruto haitadhubutu kufanya handsheki na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.
Amesema kufanya hivyo itakuwa kuenda kinyume na matakwa ya katiba ya kenya.
‘’Katika katiba ya Kenya, hakuna kifungu au chapta ya handsheki, wala rais hawezi kuwarejesha Kazi makamshna waliojiuzulu’’ alisema Gachagua.
Kuhusu kufunguliwa kwa sava ya IEBC, Gachagua amesema vile vile wao kama serikali hawajui mahali sava hiyo inapatikana na wangependa kujua ilipo.
‘’Tunataka hata sisi kujua hii sava ya iebc iko wapi. Hatujui hii sava raila atanafuata iko wapi. Hata sisi tunataka kujua iko wapi’’ aliongeza kusema Gachagua
Mojawapo ya mambo yanayochochea maandamano nchini yanayoongozwa na azimio ni kushinikiza kufunguliwa kwa sava ya IEBC.
Gachagua alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi ya mpango wa mafafuzo kazini na huduma ya umma nchini ambayo ilihudhuriwa na rais William Ruto ambapo rais alisema zaidi ya vijana 20,000 watafaidika kwa mradi huo wa serikali kuanzia mwaka ujao
Mwaka huu pekee vijana zaidi ya elfu 3 wamekwisha faidika na mradi huo