Home » Harmonize Amsifu Jay Melody
Jay Melody

Mmiliki wa lebo ya Kondegang anayetamba kwa sasa na kibao cha Single Again, Harmonize amemsifu msanii mwenza kutokea Tanzania Jay Melody kwa kuwa na ubunifu wa kukonga mioyo ya wanawake katika utunzi na uimbaji wa kazi zake za mUziki.

 

SOMA PIA:Hatimaye Davido Aiachia Timeless

 

Kupitia ukurasa wake wa Instastory, Kondeboy alimnadi Jaymelody kwa kuandika ya kuwa:

 

“Hata mwamba usipoelewa watoto wazuri watakuelewesha hutumii nguvu kabisa”

 

Kwa sasa Jay Melody ni kati ya wasanii bora zaidi nchini Tanzania huku akianza kama mwandishi wa nyimbo kwa wasanii mbalimbali akiwemo Nandy na sasa ameamua kutumia kipaji chake hicho cha uandishi kujinufaisha zaidi.

 

Ujumbe wa Harmonize kwa Jay Melody

 

Pia baada ya kumwaga sifa hizo, Jay Melody naye amemshukuru na kuandika ya kuwa pia kazi ya wawili hao itakayo toka itakuwa nzuri pia kwa kuandika

 

 

Asante sana My brother Jeshiii,Naamini hata balaa letu linalokuja litakuja kutengeneza historia kwenye Game.

 

Katika kumpatia maua hayo Jay Melody, ikumbukwe ya kuwa wimbo wa Sawa kutoka kwa msanii huyo pia ni moja kati ya mfululizo wa ngoma zake kali kuziachia ikiwemo Nakupenda, Sugar pamoja na Nitasema, ambazo zote zimekuwa kivutio kikubwa cha wadada wengi haswa wale watumiaji wa mitandao ya Ticktok pamoja na Snapchat.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!