Home » Pope Francis Kuondoka Hospitalini Jumamosi

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis anatarajiwa kuondoka hospitalini siku ya Jumamosi yaani kesho tarehe 1 Aprili na huenda akashiriki sherehe za wiki Takatifu ya mtende ya kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Pasaka.

 

 

Haya yamesemwa leo na Kadinali mmoja  katika makao makuu ya Vatican. Kwa sasa, Papa Francis anaendelea kupata nafuu katika hospitali moja Italia.
Awali taarifa zilisema Papa amekuwa na usiku wa pili mtulivu hospitalini akipokea matibabu baada ya kupata matatizo ya kupumua.

Taarifa zaidi kutoka Vatican inasema Papa Mtakatizi ni mchangamfu na anaweza kula, kusali na kufanya kazi katika chumba chake maalum cha matibabu kilichoko ghorofa ya kumi ya hospitali ya Gemelli mjini Roma.

 

Iliesemekana kwamba Papa Francis alipelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi baada ya kulalamikia matatizo ya kupumua ila baadaye wahudumu katika hospitali hiyo walisema alikuwa ameambukizwa ugonjwa huo wa mkamba (crotch)

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!