Home » Hatimaye Davido Aiachia Timeless
Davido aiachia Timeless

 

Nyota wa muziki wa Afrobeats kutokea Nigeria Davido hatimaye ameiachia Albumu yake aliyoipa jina la Timeless siku ya Ijumaa ya Tarehe 31 mezi Machi.

 

SOMA PIA: Raynanny Atumia 70M Kwa Video Yake Mpya

 

Ujio wa Timeless ulichukua muda mrefu haswa mara baada ya pigo lililompata msanii huyo la kumpoteza mtoto wake wa kiume na kupelekea kuuahirishwa kwa kazi hiyo iliyosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki.

 

 

 

Albumu hiyo ya Timeless ni Albumu ya nne kuachiwa na msanii huyo mwenye mafanikio lukuki ikiwemo tuzo za AFRIMA huku kipaji chake cha muziki kikimfanya azidi kujulikana kumataifa na kukuza jina lake.

Sambamba na hayo yote pia moja kati ya yaliyofahamika wakati wa hatua za kutoa albumu ni pamoja na ndoa ya Davido pamoja na Chioma ambayo ilikuwa mkanganyikoni endapo ilifanyika. Kwa taarifa kutoka kwa msanii huyo amekubali kwa sasa yeye ni mume wa mtu na hakuna siri tena.

 

SOMA PIA:Burna Boy Kutumbuiza Katika Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya

 

Timeless ni kazi yenye jumla ya ngoma 17 ambazo pia wasanii walioshirikishwa ni pamoja na Skepta, Asake, Focalistic, The Cavemen pamoja na mwanamama mashughuri wa muziki kutokea nchini Benin Angelique Kidjo

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!