Gor Mahia Yaimarisha Kikosi Chake

Gor Mahia imewasajili wachezaji nane wapya msimu huu kuipasha makali kikosi chake.
Usajili huu unatokea baada ya FIFA kutoa marufuku iliyokuwa imewekewa Gor Mahia ya kutosajili wachezaji baada ya kukiuka kanuni kadhaa ya soka kama vile kufeli kuwalipa baadhi ya wachezaji wao wa kitambo marupurupu yao pamoja na mahitaji mengine ya makubaliano wakati wa usajili.
Wachezaji waliosajiliwa ni mshambulizi Patrick Kaddu kutoka klabu ya Kitara Ya Uganda. Kaddu tayari ameonyesha uwepo wake kati ya mabingwa wa kenya baada ya kufunga mabao tatu katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Vihiga United.
Wengine ni mlinzi Silvester Owino kutoka Kakamega homeboyz, Emery Bayisenge kutoka klabu ya saif Sportif ya Bangladesh, Bryson Wangai kutoka Bongonaya fc na mganda shafik Kagimu.
Wengine ni Gilbert Otieno, Perminas Ochol na Boniface Otieno wote kutoka klabu ya vijana ya Gor Mahia.
Nao Police Fc wamewasajili, baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya harambee stars wakiwemo Abud Omar, Patrick Matasi, David ‘’Cheche’’ ochieng na Derrick Otanga.