Home » Mkurugenzi Wa DCI Amin Mohammed Ajiunga Na Upelelezi Wa Kifo Cha Mwathi

Mkurugenzi Wa DCI Amin Mohammed Ajiunga Na Upelelezi Wa Kifo Cha Mwathi

“Bw. Amin alijiunga na timu ya wapelelezi wakati wa ujenzi upya wa eneo la tukio katika Redwood Apartment kabla ya kufukuliwa kwa mwili iliyoratibiwa siku ya Ijumaa, 31 Machi 2023,” taarifa ilisoma.

 

DCI inalenga kubaini mapungufu ambayo ufukuzi wa mwili unatarajiwa kutoa majibu punde tu uchanganuzi utakapokamilika.

 

 

Bw Amin amewahimiza  wapelelezi wanaohusika na kesi hiyo ambayo imekuwa ya kitaifa kufanya uchunguzi wa kina ili kuhakikisha kwamba ukweli na haki zinapatikana.

 

“DCI inawahakikishia familia na wanajamii kwamba hatimaye, haki itapatikana,” taarifa ilisoma.

 

Mapema wiki hii, mahakama kuu iliipa polisi na wapelelezi idhini ya kufukuliwa kwa mwili wa kinda huyo baada ya mianya na pengo kadhaa kutokea wakati wa upelelezi.

 

 

Siku ya Jumapili, Inspekta Jenerali wa polisi Japhet Koome, alitangaza wapelelezi wanapanga kuufukua mwili wa marehemu Geoffrey Jeff Mwathi kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu kifo chake.

 

Koome alisema wamepata mapengo katika tukio hilo na hivyo wanahitaji kuufukua mwili wa marehemu ili kusaidia katika uchunguzi wao.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!