Home » Afisa Wa polisi Aliyejeruhiwa Wakati Wa Maandamano ya Azimio Huko Kisumu Afariki Hospitalini

Afisa Wa polisi Aliyejeruhiwa Wakati Wa Maandamano ya Azimio Huko Kisumu Afariki Hospitalini

Afisa wa polisi ameaga dunia baada ya majeraha aliyoyapata wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yaliyofanyika katika eneo la Juakali kaunti ya Kisumu jana Alhamisi.

 

Koplo Ben Oduor, ambaye alihudumu katika Kituo cha Polisi cha Keroka katika Kaunti ya Nyamira, alikuwa akilinda amani katika eneo la Jamia Supermarket alipozidiwa na waandamanaji ambao walimshambulia.

 

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kisumu, Alphonse Wambua ameambia wanahabari kwamba afisa huyo aliyejeruhiwa alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha Hospitali ya Aga Khan mwendo wa saa nne usiku lakini kwa bahati mbaya aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!