Koome Apongeza Polisi Licha Ya Kuwavamia Wanahabari
Licha ya kutangaza kuwa afisa mmoja wa polisi aliuawa wakati wa maandamano ya kupinga serikali yaliyoongozwa na Raila Odinga siku ya Alhamisi, inspekta generali wa polisi Japhet Koome hakuguzia au kulaani mashambulizi ya polisi kwa wanahabari.
Baadhi ya wanahabari walijeruhiwa vibaya wakati wa maandamano baada ya kurushiwa vitoza machozi wakiwa ndani ya gari wakipeperusha yaliyokuwa yakijiri wakati huo.
Katika taarifa yake kali kwa vyombo vya habari, Koome alifeli kutambua uwepo wa wanahabari au kutangaza iwapo kuna mwananchi wa kawaidi aliyejeruhiwa au kuuawa wakati polisi alipokuwa akiwakabili wanaandamanaji siku ya alhamisi maeneo ya Pipeline na Imara Daima.
Badala yake Koome ametangaza Kuwa afisa mmoja wa polisi aliiuawa na wengine 20 kujeruhiwa vibaya walipowafukuza waandamanaji waliokuwa wakizua vurugu wakiwa wamebeba vifaa butu wakati wa maandamano
Aidha, inspekta huyo wa polisi amedai wakati wa maandamano, mali ya thamani isiyojulikana iliharibiwa baada ya kundi la wahuni kuharibu mali ya kibinafsi ya watu.
Koome amehakikishia taifa na umma usalama wao na kusema kuwa polisi watafanya kila wawezalo kuwakamata wahuni.
Haya yanajiri baada ya afisi za chama tawala cha UDA kuvamiwa kwa kuchomwa kaunti ya siaya. Mali ya wananchi yaliharibiwa maeneo kadhaa ya kaunti ya Nairobi, na vile vile vifaa kuharibiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Jaramogi Oginga Odinga , Kisumu.