Home » Nyota Benson Omala Amechujwa Katika Kikosi Cha Harambee stars

Nyota Benson Omala Amechujwa Katika Kikosi Cha Harambee stars

Nyota wa Gor mahia Benson Omala amechujwa katika kikosi cha harambee stars kitakachoshiriki mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Iran ambayo imepangwa kuchezwa Machi 28 mjini Tehran.

 

 

wengine walitemwa na Mkufunzi Engin Firat ni pamoja na kiungo wa Sweden Collins Sichenje na mshambuliaji mzoefu Masud Juma, ambaye kwa sasa yuko Saudi Arabia kwa mkopo, pamoja na wachezaji wawili wa Bandari wa Mohammed Siraj (beki wa kushoto) na beki wa kati Andrew Juma, Joseph Mwangi, hassan Beja wa Nzoia Sugar ,Mlinda Lango Wa AFC Leopards Levin Opiyo Alvin Mangeni wa Police FC na Mourice Ojwang wa KCB.

 

 

KIKOSI KAMILI

Makipa: Patrick Matasi (Polisi wa Kenya), Ian Otieno (Zesco), Bryne Odhiambo (KCB).

 

 

Mabeki: Joseph Okumu (Gent), Brian Mandela (Sundowns), Johnstone Omurwa (Estrela), Eric Ouma (AIK), David Ochieng (Mathare United), Daniel Anyembe (Viborg), Daniel Sakari (Tusker), Abud Omar (Kenya Police )

 

 

Viungo: Amos Nondi (Ararat), Richard Odada (Philadelphia Union), Teddy Akumu (Sagan Tosu), Alpha Onyango (Gor Mahia), Kenneth Muguna (Azam), Abdallah Hassan (Bandari), Duke Abuya (Kenya Police), Wilkims Ochieng (FC Koper), Victor Omune (AFC Leopards).

 

 

Washambuliaji: Elvis Rupia (Police FC), Alfred Scriven (IL Hodd), Michael Olunga (Al Duhail).

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!