Home » ‘Mimi Ni Mtu Bora Sasa,’ Cristiano Ronaldo Akiri Baada Ya Kuhama Man U

‘Mimi Ni Mtu Bora Sasa,’ Cristiano Ronaldo Akiri Baada Ya Kuhama Man U

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo amesema kuwa sasa ni mtu bora zaidi baada ya kuondoka Manchester United.

 

Ronaldo aliondoka kwa Mashetani Wekundu Januari mwaka huu kufuatia mahojiano yake yenye utata na mtangazaji wa Uingereza Piers Morgan ambapo alifichua mambo ya ndani ya klabu hiyo hadharani.

 


Akizungumza katika mahojiano nchini Ureno, kabla ya mapumziko yao ya kimataifa, mshambuliaji huyo amekiri kuwa na kipindi kibaya katika maisha yake ya soka alipokuwa United.

 

“Wakati mwingine inabidi upitie mambo mengine kuona nani yuko upande wako, sina tatizo kusema nilikuwa na kipindi kibaya lakini hakuna muda wa kujuta,” alisema.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!