Home » Alinur Mohamed Amzawidi Kevin Mboya

Alinur Mohamed amemzawadia Kevin Mboya Ksh. 700,000 kama alivyoahidi.

 

Ikumbukwe kwamba Alinur Mohamed alikutana na Kevin Mboya, akamzawadia pesa na safari yenye malipo kamili ya kwenda Dubai.

 

Alinur alikuwa ameahidi kumpa Kevin zawadi siku chache baada ya kugonga vichwa vya habari kwa kusafiri kutoka Nairobi hadi Kwale kum-surprise mpenzi wake siku yake ya kuzaliwa.

 

Mambo hata hivyo hayakuenda sawa na alirudi nyumbani akiwa ameumia moyoni huku tetesi zikiwaka mtandaoni kuwa huenda alimpata mpenziwe na mwanaume mwingine, akiwa amebeba shada la maua aliyomnunulia.

 

Kisa chake kilienezwa kwenye mitandao ya kijamii na kupitia mahojiano kadhaa, Wakenya waliweza kuelewa uchungu wake.

 

Mwanasiasa na mfanyabiashara huyo aliahidi kumzawadia Mboya Ksh 700k na safari ya kwenda Dubai kumsaidia katika hali ya huzuni.

 

“Nilitabiri mambo hayaendi sawa kwa mtoto huyo Kevin Mboya na baada ya kutazama video yake kwenye akaunti zake za kijamii, nimethibitisha hofu yangu, anyway yaliyopita si ndwele namtafuta naenda kumlipia likizo yake ya wiki moja. huko Dubai na nimpe KSH. 700k kwa matumizi yake.”

 

Zawadi hiyo hata hivyo ilichukua muda na tangu Januari 29 Kevin alikuwa akitumai kwamba Alinur angetimiza ahadi yake. Jana Kevin alichapisha kwenye mitandao ya kijamii kuwa bado hajapokea pesa zozote alizoahidi mfanyabiashara huyo.

 

“Ni mwezi mmoja wiki mbili na siku mbili sasa tangu Mh Alinur atoe ahadi hii bado hajatimiza, kila ninapoenda watu wanadhani nina pesa kwa sababu wanaamini nina KSH 700K kila siku nimealikwa kwenye Harambee. Marafiki na familia yangu hunipigia simu kila siku.”

 

Wengine walimkosoa kwa kudai kwa ujasiri ahadi ambayo mtu alimpa badala ya kungoja, na wengine wakimtaka atafute pesa zake mwenyewe.

 

Jana , Alinur alichapisha kuwa kupitia mtandao wake kuwa Alnur alitimiza ahadi yake na pia alimhakikishia Kevin Mboya kuwa kuna maisha baada ya kukataliwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!