Home » Vera Sidika Amshutumu Amber Ray Kwa Kuiga Wazo Lake

Vera Sidika amemkashifu sosholaiti mwenzake Amber Ray kwa kuiga wazo lake la kufichua jinsia mtoto wake.

 

Kupitia insta stories, Vera alisema yeye huwa anaandaa karamu bora zaidi na ubunifu wake unamfanya aonekane bora.

 

Vera Sidika alifichua kuwa sherehe yake ya kufichua jinsia ya mtoto wake ilifanyika tarehe 14 Disemba, 2022 na baadhi ya watu mashuhuri wa hali ya juu walijua kuihusu.

 

Vera pia amesambaza screenshots za mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii akidai kwamba Amber alim-copy.

 

Mama wa mtoto mmoja alishiriki picha na video za jinsia ya mtoto wake zinaonyesha mialiko ya sherehe, helikopta, ziwa view na pia mumewe Brown Mauzo alimwaga Ksh 150,000 kama Kennedy Rapudo alivyomfanyia Amber Ray.

 

Wiki iliyopita Katika kipindi cha moja kwa moja na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii, wengi walishiriki jinsi Amber alivyom-copy kutoka kwa mialiko ya Lake view na vitu vinginevyo.

 

Baadhi ya mashabiki walisema Amber anamchukia Vera lakini alina-copy wazo lake.

 

Mwaka jana Amber alifufua beef yake na Vera kwa kusema Vera ni rafikli feki na hana moyo safi.

 

Mzozo huo ulidaiwa kuchochewa na Vera kutoka kimapenzi na Brown Mauzo ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Amber miaka michache iliyopita.

 

Vera hata hivyo alikanusha madai hayo akisema kuwa Amber Ray na Brown Mauzo walikuwa washirika wa kibiashara.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!