Home » Diamond Platinumz Ambadilishia Naseeb Junior Diaper

Staa wa bongo fleva nchini Tanzania Diamond Platinumz amewaacha mashabiki wake wakishangazwa na jinsi anavyofurahia ulezi wa mwanawe.

 

Mwanamuziki huyo alishiriki video akibadilisha Diaper ya mwanawe Mkenya Naseeb Junior na alikuwa akifurahia jinsi kijana huyo alivyokuwa akipinga kuvalishwa.

 

Naseeb Junior ni mtoto wa Diamond Platinumz na mwimbaji wa Kenya Tanasha Donna. Mvulana huyo kwa sasa anatumia wakati mzuri na baba yake nchini Tanzania.

 

Hivi majuzi Diamond alihudhuria hafla ya rafiki yake akiwa ameambatana na mwanawe na mashabiki waliipenda. Mwimbaji huyo alitoka kwenye gari lake la Rolls Royce hadi nyumbani kwa Haji Manara akiwa amevalia kanzu zinazofanana na mtoto Naseeb.

 

Picha alizochapisha Diamond kwenye mitandao ya kijamii ziliibua hisia tofauti kwenye ukurasa wake wa Instagram huku wengi wa marafiki na mashabiki wake wakimwita Naseeb Junior ‘Young Lion’.

 

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond kukaa na mwanawe tangu kugombana kwao na Tanasha. Mwaka jana, Diamond alitumia muda mwingi na mtoto na Naseeb Junior mwenye umri wa miaka 2 huku Tanasha akiwa Ulaya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!