Home » Jeff Mwathi Aliuawa, DCI Wakanusha Madai Kuwa Alijiua.

Maafisa wa upelelezi kutoka kwa kurugenzi wa Upelelezi wa Jinai DCI wamethibitisha kuwa marehemu Jeff Mwathi hakujiua kama ilivyodaiwa awali.

 

DCI ilikamilisha awamu ya kwanza ya uchunguzi jana na kufichua kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 23 aliuawa.

 

Kulingana na ripoti , ushahidi uliokusanywa na upelelezi ulionyesha kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 aliuawa ndani ya nyumba hiyo kabla ya kurushwa kutoka paa la nyumba anayoishi DJ Fatxo.

 

Kulingana na ripoti ya awali ya wapelelezi wa DCI, kulikuwa na ugomvi katika nyumba ya DJ Fatxo na dalili za wazi za mapambano ambayo yanaashiria uwezekano wa vita kabla ya kifo cha Jeff.

 

Awali Jeff aliripotiwa kuruka kutoka orofa ya 10 ya nyumba ya DJ Fatxo huko Kasarani.

 

DCI ilichukua udhibiti wa uchunguzi katika kituo cha polisi cha Kasarani baada ya waziri wa usalama Kithure Kindiki kuagiza uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.

 

Awamu ya pili ya Uchunguzi wa Kifo cha Jeff itahusisha mahojiano ya mashahidi katika afisi za DCI.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!