Azziad Nasenya Aonyesha Mabadiliko Ya Ajabu Baada Ya Kupambana Na Chunusi
Malkia wa Tik Tok wa Kenya Azziad Nasenya amewaacha mashabiki wakishangaa baada ya kusambaza picha za uso wake alipokuwa akisumbuliwa na chunusi mwaka mmoja baada ya kuanza matibabu.
Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Azziad anaonyesha uso wake alipokuwa akipambana na milipuko ya chunuzi, uwekundu na hata kupotelea kwa uso laini ulio wazi akionyesha anapona mara kwa mara kutokana na chunusi ambazo zilikuwa hazidhibitiki.
Mwaka jana, alifafanua kwamba alipambana na chunusi na hyperpigmentation kwa muda mrefu.
Katika kuanza safari yake ya uponyaji, alimtembelea daktari wa ngozi huku akiwa thabiti katika utaratibu wake wa kutunza ngozi.
“Nilimtembelea daktari wa ngozi na tukatathmini na kugundua kuwa chunusi yangu ni ya kimaumbile, mama yangu na shangazi walikuwa nayo.”
“Ngozi yangu ilisafishwa tukielekea mwisho wa mwaka.. Sikujua kwamba hali hiyo ingerudi kuwa mbaya zaidi. Januari 2021 ilirudi kidogo kwenye paji la uso wangu. Nilidhani. ilikuwa mzaha lakini ilirudi na mbaya zaidi.”
“Nilienda kumuona huyu daktari wa ngozi, anafanya facials kila mwezi, akaniambia nina ngozi ya mafuta natakiwa nirudi nyumbani nikajue vichochezi vyangu ni nini. Kwa mwezi huo wa kwanza niligundua Nina ngozi ya protini nyingi.”
Nyota huyo wa Tik Tok alisema anajivunia jinsi ngozi yake inavyoimarika. Pia alitoa vidokezo kwa watu wanaoshughulika na chunusi.
“Imekuwa safari. Kwa yeyote anayeshughulika na chunusi vidokezo vichache. Watu watasema lazima uwe na pesa, huu ni si ukweli. Tumeona watu wengi ambao wana ngozi nzuri lakini hawana pesa, mwenye pesa na ngozi yenye texture pia usisikilize online self proclaimed dermatologist maana kila mtu atataka kukupa dawa ufanye nini usifanye watu watakuwa wanakuonea na watakuja na sababu zozote kwa nini una chunusi.Usisikilize muone mtaalamu upate usaidizi maana watu wanaweza kuwa wajinga sana kuhusu hii mada,kuwa mvumilivu upate kinachofaa kwa ngozi yako.Sote ni tofauti na tuna aina tofauti za ngozi😊.”