Hit Maker Wa ‘Upo Nyonyo’, Akana Madai Ya Kuboresha Makalio Yake

Msanii wa muziki wa bongo fleva anayekuja kwa kasi nchini Tanzania, Saraphina Michael anayefahamika kwa jina la Phina sasa anavuma Afrika Mashariki kwa madai ya kufanyiwa upasuaji ili kujenga umbo lake.
Akizungumza katika mahojiano, Phina alisema mwili wake haujafanyiwa taratibu zozote na kuongeza kuwa ana mwili asili.
Alisema kuwa nguo za kubana alizokuwa amevaa wakati wa onyesho lake zilimfanya aonekane kama mwenye ameongezakitu kwenye makalio yake.
“Napuuza trolls zote, Mungu alichukua muda wake kuniumba. makalio yangu ni ya asili. Nina amani kwa sababu najua ni kweli.”
Phina pia anavuma sana katika muziki wa Afrika Mashariki. Ametoa EP mpya yenye nyimbo tatu.
Mwimbaji huyo wa Upo Nyonyo ana nyimbo tatu mpya: Zinduna, Smile na Rara akiwa amemshirikisha Juma Jux.
Kipaji cha Phina kilidhihirika katika shindano la Bongo Star Search baada ya kuibuka mshindi katika shindano hilo.