Evans Kidero Awaongoza Viongozi Kadhaa Kukigura ODM Na Kujiunga Na UDA
Gavana wa zamani wa Nairobi Evans Kidero amewaongoza Viongozi kadha kutoka mkoa wa nyanza kukigura chama cha ODM na kujiunga na chama cha UDA.
Wamesema uamuzi wa kuingia katika chama tawala ni kuhakikisha mkoa huo hauwachwi nyuma kimaendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari punde tu baada ya kutia sahihi na chama cha UDA, Kidero amesema serikali ya rais William Ruto ina maono mazuri kwa wakenya wote.
Aidha, Kidero amepuulizia mbali dhana kwambaNyanza ni eneo la mtu fulani akisema hilo ni dhana potovu ya kisiasa.
Ameongeza kusema hao kama viongozi hawatokubali jamii ya watu wa Nyanza kutumiwa vibaya na kukashifu tangazo la Raila odinga la kuitisha maandamao inayoratibiwa kuanza wiki ijayo .
Akiwakaribisha chamani, katibu mkuu wa UDA Clephas Malala amesema Milango ya chama hicho kiko wazi na kila mtu atapewa nafasi sawa ya kujieleza.
Baadhi ya viongozi waliotangaza kukihama ODM ni waliyekuwa magavana Jack Ranguma wa Kisumu na mwezake wa Migori Okoth Obado.
Wengine ni aliyekuwa seneta wa Kisumu Fred Outa, mwakilishi wa zamani wa akina mama Rose nyamunga, waliyekuwa wabunge Ken obura, Ken nyagudi, Omondi Anyanga, John Pesa, Nicholas Gumbo na Martin Ogindo wa rangwe.
Aliyekuwa msemaji wa polisi Charles Owino vile vile ni miongoni mwa viongozi walioitaliki chama cha chungwa.