Rais William Ruto Atangaza Uchimbaji Upya Wa Mabwawa Ya Arror Na Kimwarer
Rais william Ruto ametangaza kuanzishwa upya kwa uchimbaji wa mabwawa ya Arror na Kimwarer katika kaunti ya Elgeyo Marakwet na lile la Itare maeneo ya Kuresoi, kaunti ya Nakuru
Rais alitangaza hayo baada ya kukutana na kufanya kikao na rais wa Italia bwana Sergio Mattarella ambaye yuko nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu ya kikazi.
Mabwawa haya matatu yalizua utata mkali wa ufisadi na kisiasa katika serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kupelekea aliyekuwa waziri Henry Rotich kufunguliwa mashtaka kortini.
Hata hivyo, Ruto amesema mikakati kabambe imewekwa ya kuyachimba mabwawa ya Arror, kimwarer na itare baada ya makubaliano mapya kuafikiwa
Rais mastaafu Uhuru Kenyatta mwaka wa 2019 alifutitia mbali kandarasi ya uchimbaji bwawa hizo baada ya kubainika pesa zilifujwa katika mradi huo.
Ruto pia ametangaza serikali ya Kenya na Italia imeafikiana kuondoa kesi iliyokuwa mahakamani ya kufutitia mbali kandarasi hiyo na badala yake viongozi hao wamekubaliana kujengwa mabwawa ya kisasa litakalogharimu bilioni 66.