Home » Benachi Atoa Albamu Mpya

Benson Ongachi almaarufu Benachi, ametoa albamu yake ya ‘Not Alone’, ya nyimbo 13 ambazo ina callabo mbili na Moji Shortbaba na Guardian Angel.

 

Akizungumza na wanahabari, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alisema ni jinsi Mungu alivyomshikilia katika nyakati ngumu, “hasa nyakati ngumu, ambapo nilifikiri kuwa peke yangu, lakini Mungu alikuwa karibu nami wakati wa giza.” alisema.

 

“Yote ni juu ya kuwakumbusha waumini na Wakristo kwamba Mungu yuko karibu nao kila wakati.”

 

Alieleza kutengenezwa kwa albamu hiyo kuwa ni neema.

 

“Kusema kweli, sikuwa na changamoto kwenye albamu hii, kuna neema katika albamu hii. Watayarishaji wote walishirikiana kutoa sauti na muziki bora. Big up kwa Sevil, Teddy B na Vicky Pon This. Mungu awabariki.

 

Benachi aliwashukuru mashabiki wake kwa maoni chanya.

 

“Inaonekana kana kwamba walikuwa wamekosa muziki wangu,” alisema.

 

“Watu huwa wanapokea muziki wangu vizuri sana, lakini nadhani baadhi ya watu wanafikiri kwamba niliacha kuimba kwa vile huwa sipo karibu kufanya media tour kila ninapotoa wimbo au mradi wowote. Lakini kwa wale wanaofuatilia muziki wangu, wameipokea vizuri sana.”

Alihitimisha kuwa anaona albamu hiyo ikienda kimataifa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!