Yanga, Simba Waendeleza Ubabe Ligi Kuu Ya Tanzania
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania klabu ya soka ya Young African Sports Club, bado wameendelea kusonga mbele katika baada ya kuwafunga Geita Gold Fc mabao 3-1 siku ya Jumapili.
Ushindi huo kwa Yanga ni moja kati ya thibitisho ya kujiwekea katika nafasi ya kuchukua ubingwa wa ligi kwa mara ya pili mfululizo.
Siku ya Jumamosi, nao watani wa jadi wa Yanga, Simba Sports Club, nao wamepata ushindi wa mabao 3-0 baada ya kuwapiga Mtibwa Suger kwa ushindi wa mabao yote yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza.
Dodoma jiji nao wamezidi kumsogeza Polisi Tanzania katika hatua ya kushuka daraja baada ya kumfunga siku ya Jumapili kwa magoli 2-1.
Pia siku ya Jumapili, nao Singida Big Stars wamesuluhu bao moja kwa moja dhidi ya Coastal Union waliokuwa katika uwanja wa nyumbani