Home » Mwanaume Afariki Akijaribu Kutenganisha Wanandoa Wanaopigana

Mwanamume mmoja amepoteza maisha baada ya kupigwa na kifaa butu alipokuwa akijaribu kuwatenganisha wanandoa waliokuwa wakipigana.

 

Dan Ouma alikuwa ameingilia kati baada ya jirani yake kuanza kumpiga mkewe.

 

Akithibitisha kisa hicho, chifu wa Kanyaluo Magharibi Elius Ombim amesema mwanamume kutoka kijiji cha Seme Kaloo alikuwa akichapwa viboko na mkewe na watoto wake baada ya kutofautiana kuhusu suala la nyumbani.

 

Hii ilisababisha majirani wao, akiwemo Ouma, kuingilia kati, lakini aliishia kupigwa na kufariki.

 

Aidha kulingana na taarifa alipigwa kichwani na kukimbizwa katika Hospitali ya Kadienge kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay akiwa katika hali mbaya.

 

Kwa bahati mbaya, alifariki katika kituo hicho alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

Mwili wake ulihamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Homa Bay.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!