Home » Nairobi Yaongoza Kwa Matumizi Ya Bangi, NACADA Yasema

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa uvutaji wa bangi nchini, kulingana na ripoti ya Mamlaka ya Kitaifa ya kampeni dhidi ya matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya (NACADA).

 

Kulingana na matokeo ya utafiti wa NACADA, ‘bangi ‘ imeorodheshwa ya nne kati ya dawa zinazotumiwa vibaya zaidi nchini, ikifuatiwa na pombe, tumbaku na miraa pekee.

 

NACADA inasema, Nairobi ina kiwango cha juu zaidi cha matumizi cha asilimia 6.3, ikifuatwa na Nyanza kwa asilimia 2.4 , Pwani na Mashariki kwa asilimia 1.9 na 1.5 mtawalia.

 

Kulingana na ripoti hiyo, kiwango cha kitaifa cha matumizi ya bangi ni asilimia 1.9.

 

Matumizi ya bangi yaligunduliwa kuwa ya juu zaidi kwa wanaume, kwa asilimia 3.9, huku wanawake wakiingia kwa asilimia 0.3.

 

Kulingana na NACADA, uuzaji wa pombe na dawa zingine mtandaoni umeongeza utumizi wa dawa za kulevya nchini, na hivyo kutatiza vita dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya.

 

Miongoni mwa mapendekezo ya NACADA ya kukabiliana na janga hili ni pendekezo la kufanyia marekebisho Sheria ya ADCA 2010 na Sheria ya Madawa ya Kulevya na Kisaikolojia (Udhibiti) ya mwaka 1994.

 

NACADA inatumai kuwa hii itashughulikia changamoto zinazoibuka za ukandamizaji wa usambazaji kama vile uuzaji mtandaoni na uuzaji wa vileo, dawa za kulevya na dawa zingine za matumizi mabaya.

 

Yakijiri hayo, Kanda ya Magharibi inaongoza kwa unywaji wa pombe kali ya chang’aa nchini kote pamoja na pombe za kitamaduni, utafiti kulingana na (NACADA).

 

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa matumizi ya chang’aa yameenea zaidi Magharibi kwa asilimia 11.4, ikifuatiwa na Nyanza kwa asilimia 6.3 na eneo la Bonde la Ufa asilimia 3.6%.

 

Vile vile, eneo la Kati linaongoza kwa unywaji wa pombe kali. Na huku Kaunti ya Nairobi ikiongoza kwa unywaji wa pombe iliyotengenezwa na kudhibitishwa kisheria, eneo la Kati linashika nafasi ya pili katika kitengo hicho, likiangazia unywaji pombe kupita kiasi katika eneo lenye watu wengi zaidi nchini Kenya.

 

NACADA pia imechunguza kuenea kwa matumizi ya sasa ya angalau dawa moja ya unyanyasaji, ambapo eneo la Magharibi pia liliibuka kuwa linaongoza kwa asilimia 26.4.

 

Wakazi wa mikoa ya Mashariki na Nairobi pia walipatikana kutumia angalau dawahizo kwa asilimia 20.7 na 19.2 mtawalia.

 

NACADA imebaini tatizo kubwa na linaloongezeka la matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya ambalo ilisema linahitaji kushughulikiwa.

 

Kwa ujumla nchini Kenya, pombe imepatikana kwamba inayotumiwa vibaya zaidi nchini, huku milioni 3,199,119 ya watu wakiathirika, ikifuatiwa na Tumbaku milioni 2,305,929 na watu elfu 964,737 walioathiriwa mtawalia.

 

Wakati huo huo matumizi mabaya ya bangi yanaathiri watu elfu 518,807 huku dawa zikiathiri watu elfu 60,407 kote nchini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!