Home » Mwili Wa Mwanafunzi Aliyefariki Akiogelea Nchini Australia Wawasili Eldoret Kwa Mazishi

Mwili Wa Mwanafunzi Aliyefariki Akiogelea Nchini Australia Wawasili Eldoret Kwa Mazishi

Mwili wa mwanafunzi Mkenya aliyekufa maji mwezi Februari alipokuwa akiogelea nchini Australia umetua nchini Kenya na kupelekwa Eldoret, mji alikozaliwa.

 

Sharon Jepkosgei Kigen, ambaye alitoka Moiben katika Kaunti ya Uasin Gishu, alikufa maji kusini magharibi mwa Sydney kulingana na polisi wa eneo hilo.

 

Familia ilikuwa imeomba msaada wa kurudisha mwili wake nyumbani na Wakenya wanaoishi Australia walikusanyika pia kuchangisha pesa kwa ajili ya shughuli hiyo.

 

Watu waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege wameutazama mwili kwa huzuni.

 

Mwili wa marehemu umepelekwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Eldoret tayari kwa misa ya mazishi iliyopangwa Jumanne, Machi 14.

 

Sharon Aliondoka Kenya kuelekea Australia mnamo Novemba 2022 kwa ajili ya masomo katika chuo kikuu cha Kikatoliki cha Australia-North Sydney.

 

Baada ya kuogelea na kuzama kwa msichana huyo mkenya, waokoaji waliarifiwa kuhusu alikokuwa akiogelea karibu na Georges River katika eneo la Macquarie takriban saa 3.45 jioni.

 

 

Kuzama huku kunajiri miezi 6 tu baada ya Mkenya mwingine pia kupoteza maisha katika bwawa nchini Canada alipokuwa akizungumza na mashabiki zake moja kwa moja kupitia mtandao wa Facebook.

 

 

Mnamo Agosti 2022, muuguzi wa Kenya kwa jina Helen Nyabuto alikuwa akiogelea wakati ghafla alizama kwenye video ya kutisha iliyosambaa mitandaoni.

 

Hellen, 24, alionekana akizungumza na watazamaji mtandaoni kabla ya kuogelea hadi kwenye kina kirefu cha maji na kufa maji.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!