Home » Navy Kenzo Waachilia Albamu Mpya

Wapenzi wanaounda kundi la Navy Kenzo Aika na Nahreel wamefanikiwa kuachia albumu yao ya tatu siku chache zilizopita.

 

 

Katika albumu hiyo waliyoipa jina la Most People want this (MPWT) yenye nyimbo 12 wamefanikiwa kuiachika huku kukiwa na msanii mmoja kutokea Nigeria aliyeshirikishwa ambaye ni Fireboy.

 

SOMA PIA: Zuchu Na Baraka Za Napambana Kwa Wanawake

 

Ukimya wao wa muda mrefu umeleta neema kwa Navy Kenzo baada ya Albumu hiyo ya MPWT kushika nambari moja katika jukwaa la muziki la Apple Music kwa nchini Tanzania.

 

 

Albumu ya Most People Want This pia Navykenzo wana albumu nyingine kama vile ‘Above Inna Minute’ ya mwaka 2017 pamoja na ‘Story Of The African Mob’ waliyoiachia mwaka 2020, zikiwa na mafanikio makubwa katika kundi hilo.

 

 

MPWT imesheheni nyimbo kali kama vile ‘Manzese’  ‘Madness’  ‘Don’t let go’, ‘Company’  ‘Tonight’ na nyingine nyingi bila kusahau ‘Hold on’ waliyomshirikisha Fireboy DML.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!