Home » Rapa Costa Titch Aanguka na Kufariki Dunia Jukwaani

Magwiji wa muziki kutoka duniani kote wanamuombeleza mwanamuziki kutoka Afrika Kusini Rapa Costa Tsobanoglou maarufu kwa jina la Costa Titch ambaye alizimia na kufariki wakati akitumbuiza kwenye tamasha la muziki la Ultra jijini Johannesburg usiku wa kuamkia jana.

 

Hitmaker huyo wa ‘big flexa’ alikuwa akitumbuiza moja ya nyimbo zake, ndipo alipoanguka jukwaani. Baadaye, alisimama na kuendelea na utumbuizaji lakini alilemewa na kuanguka tena na kufa.

 

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa maarufu kwa mchango wake katika muziki wa Amapiano kwa vibao kama vile ‘Big Flexa’, ‘Nkalakatha’ na ‘Activate’.

 

Mwanamuziki huyo aliyeibuka kidedea hivi majuzi alisaini mkataba na lebo ya Akon, Konvict Kulture na kushirikiana kufanya remix ya ‘Big Flexa’.

 

Costa Tsobanoglou, anayejulikana zaidi kwa jina la Costa Titch, anaripotiwa kuwa na historia ya kifafa, hali inayoathiri ubongo na kusababisha mshtuko.

 

Kifo chake ni mkasa wa hivi punde zaidi katika tasnia ya muziki ya Afrika Kusini. Katikati ya Februari, rapa maarufu Kiernan Forbes, anayejulikana kama AKA, aliuawa kwa kupigwa risasi huko Durban.

 

Pumzika kwa amani Costa Titch.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!