Home » Ten Hag Akiri Umuhimu wa Bruno United Katika Kikosi Chake

Kocha wa timu ya Manchester United amesimamia msimamamo wake juu ya kumbakisha Bruno Fernandes kuwa nahodha msaidizi wa kikosi hicho cha Mashetani wekundu akiwa sambamba na nahodha mkuu wa kikosi hicho Harry Maguire.

 

Hayo yamejiri mara baada ya United kupoteza katika mchezo wao dhidi ya Liverpool kwa kuonesha uwezo mbovu katika mchezo huo na kupelekea Mreno huyo kuingika katika midomo yya wapenzi wa soka juu ya kuvuliwa kitambaa cha unahodha wa timu hiyo.

Erik Ten Hag- Bruno Fernandes

Baada ya hayo yote kocha wa timu hiyo Eric Ten Hag amemkingia kifua mchezaji huyo kwa kueleza sababu za kuwa na imani dhidi ya mchezaji huyo huku akisema

huku Hakuna ambaye amekamilika kila mtu anafanya makosa kiukweli nina furaha kuwa na Bruno Fernandes katika timu yangu na ninafuraha kuwa naye kama nahodha wetu pamoja na Harry akiwa nje ya uwanja

Katika mchezo unaofuata Manchester United watacheza mechi yao dhidi ya Real Betis katika hatua ya 16 bora ligi ya Europa baada ya Liverpool kuwaadhibu kwa kipigo cha bao 7-0

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!