Home » Feisal Aikacha Barua ya Yanga, Atimkia Mecca
Feisal aikacha Yanga

Kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania Feisal Salum aikacha barua ya Yanga na kutimkia Mecca huku picha zikisambaa zikimuonesha mchezaji huyo akiwa anakamilisha swala La Umrah katika kukamilisha nguzo Tano za Uislamu.

Feisal aikacha Yanga

Hatua hiyo imejiri wakati ambao mchezaji hiyo akiwa amefikishiwa barua ya kuwasili mazoezini na klabu Yanga licha ya Feisal pia kuwasilisha barua katika shirikisho la soka TFF akiomba kuvunjiwa makataba wake na timu hiyo.

Jambo la mchezaji huyo wa Yanga



kusafiri kwenda nje ya nchi imeonesha kwa uwazi ya kuwa bado azma yake imesimamia kuondoka Yanga na huku akiendelea kuchukua hatua zaidi juu ya jambo hili n hata kubadili mwanasheria wa kusimamia suala hilo

 

Kwa sasa kilichobaki ni TFF kutoa majibu juu ya barua iliyowasilishwa na Feisal endapo shirikisho hilo litaamua kufuatilia upya suala  hilo au kusimamia maamuzi yao ya mwanzo

 

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!