Home » Raila Odinga Azuiwa Kuingia Katika Makao Makuu Ya DCI

Kiongozi wa Azimio Raila leo Jumanne ametakiwa kuondoka kwenye lango la makao makuu ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai DCI huku wafuasi wake wakiendelea kuzua hali ya kutatanisha.

 

Makumi ya wafuasi wa Azimio wamekusanyika karibu na Mazingira House, Barabara ya Kiambu.

 

Kiongozi huyo wa upinzani amezuiwa kuingia hadi afisi kuu za DCI ambako aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i anarekodi taarifa.

 

Muda mfupi baada ya Raila kuwasili, Mkuu wa Operesheni za Polisi katika DCI Said Kiprotich na Mkuu wa Upelelezi Eliud Lagat walijitokeza kuzungumza na Raila mlangoni.

 

Walimweleza Raila kuwa uwepo wake katika makao makuu ya DCI haukukubalika kwani unazua mvutano usio wa lazima.

 

Kwa sasa Matiang’i yuko katika afisi kuu za DCI ambapo anarekodi taarifa kuhusiana na madai ya kuvamiwa nyumbani kwake Karen mwezi uliopita.

 

Raila kwa gadhabu amewakashifu maafisa wa polisi waliomzuia kufika katika makao makuu ya DCI.

 

“Mimi ni afisa wa umma, siwezi kuzuiliwa kuingia kwa afisi ya umma, lazima nionane na mkurugenzi, ni sheria gani hiyo,” Raila alidai.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!