Home » Bifu Limeisha? Diamond Platinumz Adokeza Kupenda Ngoma Hii Ya Ali kiba

Nyota wa muziki kutokea lebo ya WCB Nasib Abdul maarufu kama Diamond platnumz, ameingia kwenye vichwa vya habari Tanzania baada ya kuonesha kukubali na kuipenda ngoma ya Asali ya msanii Ali Kiba.

 

 

Kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki Tanzania, Diamond Platnumz na Ali Kiba wamekuwa wakitafsiriwa na vyombo vya habari, mashabiki na wadau wa burudani kama mahasimu wa kwenye muziki.

 

 

Kwenye ukurasa wa Instagram wa Diamond Platnumz upande wa Instastory,  Diamond, aliweka picha ya ngoma ya Ali Kiba ya kuitwa Asali na kuweka neno Favourite akimaanisha ni ngoma yake pendwa, kitu ambacho wengi hawakukitegemea kutokana na uhasimu walionao kwa muda mrefu.

 

 

Bifu kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba ni la muda mrefu na mara kwa mara wasanii hao kupitia mashahiri ya ngoma zao wamekuwa wakitupiana maneno.

 

 

Akiwa kwenye mahojiano na Sporah Show mwaka 2014, Ali Kiba alidokeza kuwa mpasuko wake na Diamond Platnumz ulianza baada ya Diamond kutoa kipande alichoimba kwenye ngoma ya Lala Salama bila yeye kupewa taarifa na tangu hapo wasanii hao wawili ambao kwa sasa ni moja ya wasanii pendwa zaidi Tanzania hawakuwa na ukaribu tena.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!