Home » Wanawake Waliodhulumiwa Kericho Wahofia Kutoa Ushahidi Wakihofia Kupoteza Ajira Yao

Wanawake Waliodhulumiwa Kericho Wahofia Kutoa Ushahidi Wakihofia Kupoteza Ajira Yao

Kamati ya Bunge kuhusu Leba wikendi hii ilitembelea Kaunti ya Kericho kuchunguza madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake katika kampuni ya majani chai (Unilever) na nyingine ya James Finlay Kenya.

 

Kamati hiyo Ikihutubia wanahabari baada ya kikao cha faragha na vyombo vya usalama, uongozi wa kaunti na washikadau wengine, kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Runyenjes Erick Muchangi imefichua kuwa hakuna waathiriwa waliojitokeza kurekodi taarifa kuhusiana na tukio hilo kwa kuhofia kupoteza kazi zao.

 

Mwakilishi wa Wanawake wa Kericho Beatrice Kimei amewarai wanawake ambao walitoa ushahidi katika makala ya BBC wakidai kudhulumiwa kingono ili kujitokeza na kurekodi taarifa za kusaidia katika uchunguzi.

 

Kimei amewahakikishia wanawake hao usalama wao huku akidokeza kuwa watalindwa na hakuna hata mmoja wao atakayedhulumiwa.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji mwezi uliopita aliomba Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) kuanza uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono katika kampuni hizo mbili.

 

Agizo hilo la Haji lilijiri baada ya ripoti ya uchunguzi ya hivi majuzi ya shirika la BBC Africa ambapo wanawake wawili vibarua wa kawaida walidai kulazimishwa kulala na maafisa wa ngazi za juu katika kampuni hizo ili kupata ajira na baadaye wakagundua kuwa waliambukizwa virusi vya ukimwi na wasimamizi wao..

 

Kufikia sasa, kampuni ya James Finlay Kenya imewasimamisha kazi wakandarasi wawili baada ya kufichuliwa kwa ripoti hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!