Home » Mkewe Rais Rachel Ruto Atoa Wito Wa Suluhu Za Dharura Za Afya Ya Uzazi katika Maeneo Kame

Mkewe Rais Rachel Ruto Atoa Wito Wa Suluhu Za Dharura Za Afya Ya Uzazi katika Maeneo Kame

Mkewe Rais, Mama Rachel Ruto ametoa wito wa huduma ya haraka ya afya ya uzazi katika maeneo kame wakati wa ufunguzi rasmi wa hospitali ya Misheni ya Segera katika Eneo Bunge la Laikipia Kaskazini.

 

Wakazi wanaoishi katika maeneo hayo wanakabiliwa na changamoto nyingi za kipekee za afya na ustawi, mbaya zaidi kutokana na ukame, ambao unahitaji huduma za dharura.

 

Hosptali hiyo ilianzishwa na marehemu Mchungaji Carlton Gleason mwaka 2002 baada ya kutembelea na kuona mahitaji ya watu wa Segera.
Aidha alianzisha kliniki ya matibabu, shule, mpango wa kulisha wajane na mayatima, pamoja na hospitali hiyo.

 

Ikiwa ndiyo hospitali pekee katika eneo la kilomita 72, Hospitali ya Misheni ya Segera itatoa huduma muhimu za matibabu ambazo zitaokoa maelfu ya Wakenya na vile vile gharama ya kusafiri mbali kutafuta huduma za matibabu.

 

Aidha mama Rachel ametoa msaada wa chakula kwa wakazi walioathirika na ukame, ambao ni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40, ambapo baadhi ya maeneo yamekosa mvua kwa misimu mitano mfululizo kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

 

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Gavana wa Laikipia Joshua Irungu, Mbunge wa Laikipia Kaskazini Sarah Korere, Spika wa Bunge la Kaunti ya Laikipia Lantano Nabaala, na Kamishna wa Kaunti ya Laikipia Joseph Kanyiri.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!