Home » Raila Aorodhesha Masharti 3 Kabla Ya Kukubaliana Na Serikali Ya Rais Ruto

Raila Aorodhesha Masharti 3 Kabla Ya Kukubaliana Na Serikali Ya Rais Ruto

Kiongozi wa Chama cha Azimio Raila Odinga amefichua kuwa kulikuwa na nafasi ya mazungumzo kati ya Rais William Ruto na yeye mwenyewe licha ya ukosoaji wake wa mara kwa mara dhidi ya Serikali ya Kenya Kwanza.

 

Raila alizungumza hayo jana wakati wa mahojiano ya kipekee na runinga moja humu nchini ambapo alisikitika kuwa gharama ya maisha ni ya juu sana kwa Wakenya.

 

Waziri Mkuu huyo wa zamani pia ametaka rais ruto kufungua sava za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) pamoja na kusitisha uajiri wa makamishna wa IEBC.

 

Kulingana na Waziri Mkuu huyo wa zamani, Rais Ruto atalazimika kutimiza masharti matatu ambayo yanagusa mchakato wa uchaguzi na hali ya kiuchumi ya nchi kabla ya kukubali kufanya mazungumzo na Serikali yake.

 

Raila amekashifu zaidi mpango wa Ruto wa kusitisha ruzuku uliotekelezwa na mtangulizi wake Uhuru Kenyatta wakati wa utawala wake.
Hata hivyo, Raila Odinga amelinganisha Kenya na nchi nyingine kama Brazil, Chile, Japan, India, na Misri ambazo zilipitia mdororo wa kiuchumi duniani.

 

Zaidi ya hayo, Raila ameteta kuwa mpango wa Ruto wa kufutilia mbali Kazi Mtaani ni dharau kwa vijana waliokuwa wakipigana na ukosefu wa ajira.

 

Mnamo Jumatano, Februari 22, Raila alitoa madai sita kwa Ruto na kumpa makataa ya siku 14 kabla ya kuanza kuchukua hatua nchini kote.

 

Madai mengine yaliyoorodheshwa na Raila yalikuwa kuanzisha upya ruzuku ya chakula, kusajili watoto wote walioacha shule, kupunguzwa kwa karo na kusitisha mchakato wa kujihusisha na tume ya IEBC.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!