Home » Bei Za Unga, Umeme Na Bidhaa 4 Nyingine Za Msingi Zashuka Baada Ya Rais Ruto Kuingilia Kati

Bei Za Unga, Umeme Na Bidhaa 4 Nyingine Za Msingi Zashuka Baada Ya Rais Ruto Kuingilia Kati

Ahadi ya Rais William Ruto ya kupunguza bei ya bidhaa za kimsingi inaonekana kudhihirika kufuatia ripoti ya hivi punde ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) iliyotolewa jana Jumanne, Februari 28.

 

Huku Wakenya wengi wakihangaika na gharama ya juu ya maisha, awali walidai kupunguzwa kwa bei ya bidhaa sita muhimu kama afueni kubwa kwao.

 

Miongoni mwa bidhaa za kimsingi zilizoshuka kwa bei jana kwa kipindi cha kati ya Januari 2023 na Februari 2023 ni pamoja na unga wa mahindi ulioimarishwa na umeme.

 

Bei ya unga wa mahindi ulioimarishwa kwa kilo 2 imeshuka kwa asilimia 2.5 huku maduka mengi ya rejareja yakiuza bidhaa hiyo kwa bei ya wastani ya shilingi mia 180 kama alivyoahidi Rais Ruto.

 

Februari 23, Rais aliahidi kuendeleza hatua za kuingilia kati ili kupunguza bei ya unga wa Mahindi.

 

Bei ya umeme pia imesajili kushuka kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 2.9 na asilimia 3.7 kwa kilowati 200 na kilowati 50 mtawalia.

 

Aidha, hatua hii ilikuwa baada ya Baraza la Mawaziri kuidhinisha kuondolewa kwa kusitisha Mikataba ya Ununuzi wa Nishati (PPAs) kama njia ya kuimarisha usalama wa nishati ya taifa kwa kufungua sekta ya nishati kwa uwekezaji unaoendelea.

 

Baraza la Mawaziri pia lilifichua kuwa litapunguza bei kwa kudhibiti bei za wakandarasi huru wa kawi waliolaumiwa kwa kutoza Kenya Power kupita kiasi hatua iliyosababisha bei ya tokeni kuongezeka.

 

Pakiti ya kilo 2 ya unga wa ngano vile vile imesajili kushuka kwa bei kwa asilimia 2.4 huku wauzaji wengi wakiuza kwa bei ya wastani ya shilingi 191.

 

Sukari nayo sasa ni wastani wa shilingi mia 141 huku sukari nyeupe ikiuzwa kwa wastani wa shilingi mia 150 ambayo ilikuwa punguzo la asilimia 3.2.

 

Bidhaa zilizosajili ongezeko la bei ni pamoja na; kodi ya nyumba ya kila mwezi (asilimia 0.3), gesi ya kupikia (asilimia 4.7), machungwa (asilimia 2.8), nyanya (asilimia 7.8),na kabichi (asilimia 11.3). )

 

Mnamo Jumapili, Februari 26, Ruto alitoa ramani yake ya kuhakikisha kuwa gesi ya kupikia inakuwa rahisi kwa kila kaya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!