Familia Ya Dedan Kimathi Yataka Serikali Kutafuta Mabaki Yake

Familia ya mpigania uhuru Dedan Kimathi sasa inataka serikali ya kwanza ya Kenya kutafuta mabaki yake ili mke wake Mukami Kimathi akifariki azikwe kando yake.
Akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 66 ya kunyongwa kwake, bintiye Kimathi Evelyn Wanjugu Kimathi alikashifu kuwa ni bahati mbaya kwamba mabaki ya jamaa zao bado yamelazwa katika eneo lisilojulikana katika gereza la Kamiti ambapo alinyongwa.
Huku akionyesha matumaini, Evelyn alithibitisha kuwa ana matumaini kuwa utawala unaoongozwa na Rais William Ruto utaweza kufuatilia mabaki ya mpendwa wao kama ilivyoombwa.
Kimathi alitekwa na vikosi vya wakoloni mnamo 1955 katika kijiji cha Karunaini huko Nyeri wakati wa harakati za kupigania uhuru. Alinyongwa huko Kamiti ambapo alizikwa kwenye kaburi lisilojulikana.
Majaribio na ahadi za serikali zilizopita za kutaka kuwa na mabaki yake kufikia sasa hazijafauli.
Taarifa hii inajiri saa chache baada ya aliyekuwa mbunge wa subukia Koigi Wa Wamwere vile vile kuokezea jinsi serikali ilivyofeli kurejesha miili ya baadhi ya mashujaa hapa nchini kenya baada ya kuzikwa kusikojulikana.