Naibu Rais Rigathi Gachagua Akashifu Polisi Kusimamia Kufurushwa Kwa watu mtaa Wa Rongai Nakuru

Naibu Rais Rigathi Gachagua amekemea Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) kwa kusimamia kufurushwa kwa karibu familia mia 105 kutoka kwa kipande cha ardhi ambacho walikuwa wamekimiliki kinyume cha sheria katika kijiji cha Kiriko, Rongai, Kaunti ya Nakuru Jumatano.
Akizungumza mjini Nakuru leo hii Jumamosi alipoongoza ugawaji wa chakula cha msaada katika eneo hilo, Gachagua amebainisha kuwa polisi kwanza wamepewa mamlaka na sheria kulinda maisha na mali ya Wakenya na wala si kuangalia upande mwingine mali inapoharibiwa.
Kulingana na Gachagua, kabla ya kuwafurusha familia hizo, polisi walipaswa kujadiliana kuhusu njia za kuwahamisha kwa muda katika misingi mipya.
Naibu rais ameongeza kuwa kamanda wa polisi aliyeongoza oparesheni hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru Peter Mwanzo, amerudishwa katika makao makuu ya NPS na kwamba serikali itamchukulia hatua.