Home » Mvulana Wa Miaka 17 Azama Kwenye Mto Migori

Maafisa wa Polisi eneo la Kuria Magharibi, Kaunti ya Migori, wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mvulana wa umri wa miaka 17 aliyekufa maji katika mto Migori eneo la Masaba jana Ijumaa.

Kamanda wa polisi wa Kuria Magharibi Cleti Kimaiyo amesema mwili wa marehemu aliyetambuliwa kama Alex Ochieng ulipatikana katika mto Migori.

Kulingana na Kimaiyo uchunguzi wa awali ulibaini kuwa marehemu alikufa maji katika mto Migori alipokuwa katika msafara wa kuogelea na kuongeza kuwa marehemu alikuwa na kaka yake wakati tukio hilo likitokea.

 

Mwili huo umehamishwa hadi  chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya kumbukumbu ya Ojele kusubiri uchunguzi wa polisi pamoja na upasuaji.

Wakati uo huo, Kimaiyo ametoa wito kwa wazazi kuwazuia watoto wao kuingia mtoni ili kuepuka vifo hivyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!