Viongozi Wa Afrika Mashariki Kuzungumzia Machafuko Ya DR Congo
Viongozi wa Afrika Mashariki wamelekea Burundi lei hii Jumamosi kwa mkutano wa kilele wa kanda ulioitishwa kujadili mzozo unaoendelea mashariki mwa DR Congo.
Mazungumzo hayo yanaandaliwa mjini Bujumbura na Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo inaongoza juhudi za upatanishi ili kumaliza mapigano yanayozuka tena mashariki mwa taifa hilo kubwa la Afrika ya kati.
Taarifa kutoka taifa la kongo imesema kwamba Rais Felix Tshisekedi atahudhuria.
Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye anatuhumiwa kuunga mkono makundi ya waasi mashariki, amewasili mjini Bujumbura, pamoja na wakuu wengine kadhaa wa nchi za EAC pia.
Mkutano huo unafanyika muda mfupi baada ya ziara ya Papa Francis mjini Kinshasa, ambako alikutana na wahanga wa mzozo huo na kulaani vurugu zisizo za kibinadamu na unyama wa kikatili unaofanyika.
Wanamgambo wamekumba eneo hilo lenye utajiri wa madini kwa miongo kadhaa, nyingi zikiwa ni urithi wa vita vya kikanda ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Tangu Novemba 2021, kundi la waasi linalojulikana kama M-23 limeteka sehemu kadhaa za eneo la mashariki na kufika umbali wa kilomita kadhaa kutoka kitovu chake kikuu cha kibiashara cha Goma.
DRC inashutumu jirani yake wa Afrika ya kati Rwanda kwa kuunga mkono M23, jambo ambalo wataalamu wa Umoja wa Mataifa, Marekani na mataifa mengine ya Magharibi wanakubaliana nalo.
Aidha Wiki iliyopita, Qatar ilikuwa imepanga kuandaa mkutano kati ya Tshisekedi na Kagame, lakini wanadiplomasia walisema kiongozi huyo wa Kongo alikataa kuhudhuria.
Kadhalika Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambaye ni mpatanishi kwa niaba ya EAC, mwezi uliopita alielezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kuzorota kwa kasi ya maendeleo ukanda wa mashariki ya afrika.