Home » Waziri Miano Azungumzia Hali Ya Ukame Nchini

Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Maendeleo ya Kikanda Rebecca Miano amejibu madai ya Maseneta 14 kutoka kaunti zilizoathirika na ukame na kutaka ukame utangazwe kuwa janga la kitaifa.

 

Katika mujibu wa Miano amebainisha kuwa Kenya ni miongoni mwa nchi za Pembe ya Afrika ambazo kwa sasa zinakabiliwa na ukame wa muda mrefu kufuatia misimu mitano mfululizo ambapo mvua haijanyesha ya kutosha.

 

Akibainisha kuwa masuala yaliyoibuliwa na maseneta hao ni muhimu, hata hivyo amewahakikishia Wakenya kwamba serikali, itaungwa mkono na washirika wa maendeleo, sekta ya kibinafsi na wadau wengine wasio wa serikali.

 

Aidha, Waziri huyo amedai kuwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alitangaza rasmi ukame katika baadhi ya maeneo ya Kenya kuwa janga la kitaifa mnamo tarehe 8 Septemba 2021.

 

Zaidi ya hayo, kati ya Julai na Oktoba 2022, serikali ilitoa shilingi bilioni 1.07 kama msaada katika kaunti za Turkana, Marsabit, Mandera na Wajir chini ya Mpango wa Usalama na kukabili Njaa mpango unaotekelezwa na NDMA.

 

Hata hivyo, Waziri amekariri kuwa serikali inafanya kila iwezalo kupunguza mateso ya Wakenya walioathiriwa na ukame, japokuwa na rasilimali chache za kifedha.

 

Maseneta waliolalamika ni ikiwemo Ledama Kina wa (Narok), Ali Roba wa (Mandera), Danson Mungatana wa (Tana River), Mohammed Chute wa (Marsabit), James Lomenen wa (Turkana), Abbas Mohammed wa (Wajir), Lelegwe Ltumbesi wa (Samburu), Stewart Madzayo wa ( Kilifi), William Kisang wa (Elgeyo Marakwet), Joseph Githuku wa (Lamu), Lenku Seki ambao wanadai serikali kushughulikia suala hilo kwa dharura.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!