Home » Serikali Yarudisha Ksh.202M ya DP Gachagua

Shilingi milioni 202 na mali ya Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambayo ilitwaliwa na serikali imerejeshwa kwake.

Wakala wa Urejeshaji Mali (ARA) umesema baada ya kukusanya ushahidi mpya, walibaini kuwa fedha zilizoshikiliwa na serikalini miezi sita iliyopita hazikuwa za uhalifu na kwamba Naibu Rais ameeleza chanzo na uhalali wa fedha hizo ili kujiridhisha.

Wanadai kuwa wakati mahakama kuu ilikuwa ikitoa uamuzi wake, ushahidi huo mpya haukuwekwa mbele ya hakimu kwa vile shirika hilo halikuwa na ushahidi huo.

Leo Mahakama ya Rufa imebatilisha amri ya tofauti na iliyotolewa na Mahakama Kuu mwaka jana na pia kutupilia mbali hukumu hiyo ya Mahakama Kuu.

Hii inamaanisha kuwa pesa zilizo katika akaunti tatu katika Benki ya Rafiki Microfinance kwa jina la Rigathi Gachagua zitatolewa kwake. Vile vile, Pesa zilizo katika akaunti nyingine ya Jenne Enterprises pia zitatolewa.

Fedha hizo katika Benki ya Rafiki Microfinance, ziko katika akaunti tatu huku moja ikimiliki Ksh. Milioni 165, akaunti ya pili ina Ksh. Milioni 35 na nyingine ina ksh.773,228.

Akaunti ya nne, yenye Ksh. milioni 1,138,142, imesajiliwa kwa jina la Jenne Enterprises.

Naibu rais Gachagua alisema mwaka jana kwamba mojawapo ya ndoto zake atakapokuwa Naibu Rais itakuwa kurejesha pesa hizo baada ya serikali kutilia shaka chanzo cha Ksh. Bilioni 12.5 zilizopitia akaunti zake za benki.

Mapato hayo, Gachagua alisema, yatatumika kujenga miundombinu nyumbani kwake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!