Serikali Kudhibiti Utovu Wa Nidhamu Miongoni Mwa Wanafunzi
Huku wanafunzi wakitarajiwa kurejea shuleni kwa masomo yao ya muhula wa kwanza mwaka huu, serikali inahimizwa kubuni sheria mpya na mwongozo wa kudhibiti utovu wa nidhamu .
Akizungumza kwa niaba ya wazazi katika eneo bunge la Mogotio kaunti ya Baringo, Aaron Chemaina ambaye ni mshikadau wa elimu anasema haki za watoto na haswa marufuku ya kutoa adhabu kwa kiboko zimefungua milango kwa baadhi ya watoto kukataa shule, na pia kutoheshimu wazazi wao na walimu.
Chemaina anasema kutokana na sheria kuhusu haki za watoto, wazazi wengi na pia walimu kwa wakati mwingine wanashindwa kuwadhibiti wanafunzi.