Walaghai Wa Mihuri Bandia Ya KRA Wakamatwa

Kufuatia oparesheni inayoendelea dhidi ya bidhaa ghushi nchini, maafisa wa upelelezi wameendeleza msako dhidi ya washukiwa wa kutengeneza mihuri bandia ya Mamlaka ya Ushuru Nchini (KRA) na kuwakamata washukiwa sita.
Peter Mburu, James Kigera, Frankline M’Mburia, Mary Wanjiku, Titus Ndegwa na Jane Muthoni wamekamatwa wakiwa katika maeneo tofauti ya jiji la Nairobi na kupatikana na mihuri bandia ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na pia Mamlaka ya Mapato ya Uganda.
Mmoja wa washukiwa Titus Ndegwa ambaye alikamatwa katika makazi yake huko Thindigua katika kaunti ya Kiambu, alipatikana kuwa mmiliki wa silaha zisizo za kiraia na bunduki yake ya Glock, iliyokuwa na risasi 9 ilichukuliwa
Washukiwa hao kwa sasa wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga wakishughulikiwa ili kufikishwa mahakamani.