Home » Jovial arushia wafanyibiashara vijembe

Msanii Jovial Katika ubora wake

Na Burare Kennedy

Msanii nyota nchini Jovial ameshindwa kuwavumilia wafanyibiashara wanaotumia picha za mastaa kwenye matangazo bila ridhaa yao.

Kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram mkali huyo wa sauti amewapa somo wafanyibiashara sampuli hiyo kwa kuwaita wabahili wa kutoa michongo kwa wasanii licha ya kuwa wanalipwa mkwanja mrefu na makampuni tofauti kufanikisha shughuli hiyo.

Hitmaker huyo wa “Mi Amor” amehapa kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakayejaribu kutumia picha yake bila idhini kwenye matangazo ikizingatiwa kuwa ametumia pesa nyingi kuitengeneza brand au chapa yake.

Hata hivyo amewataka walimwengu kuacha kasumba ya kutumia njia ya mkato kufanikisha michongo yao na badala yake amewaasa kutoa riziki kwa wenzao kutokana na uhitaji wa watu duniani kutaka kufanikisha ndoto zao maishani.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!