Home » Baha aapa kumshtaki aliyehusika kusambaza video chafu za Georgina

Baha katika pozi la mahaba na mahanjam na mpenzi wake Georgina

Na Burare Kennedy.

Muigizaji Tyler Kamau Mbaya almaarufu Baha kutokana na kipindi ‘Machachari’ amemhakikishia mpenzi wake Georgina Njenga kuhusu mapenzi yake makubwa kwake licha ya video yake chafu ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hivi majuzi, wapenzi hao waligeuka kuwa gumzo mitandaoni baada ya video zinazodaiwa kuwa za Bi Georgina akicheza akiwa uchi kuvujishwa.

Baha hata hivyo ameweka wazi kuwa tukio hilo halijatikisa mahusiano yake hata na kufichua kwamba bado wako pamoja.

Baha alifichua kuwa mzazi huyo mwenzake bado anaendelea vyema licha ya hali ya kutatanisha inayomzunguka kwa sasa.

“Yuko shwari, hata niko naye,” alisema.

Wakati huo huo, muigizaji huyo kijana alifichua kwamba mikakati ya hatua za kisheria dhidi ya aliyevujisha video hizo inaendelea.

Ingawa hakutoa maelezo mengi, Baha alifichua kwamba wanajiandaa kumshtaki mhusika kwa aibu aliyomletea mpenziwe. 

Hapo awali, Bi Georgina alikuwa amedai kwamba mpenzi wake wa zamani ndiye aliyehusika katika uvujishaji wa video hizo chafu.

Wakati akimjibu mwanablogu wa hapa nchini, alidokeza kuwa mpenzi wake huyo wa zamani  hakufurahishwa na uhusiano wake na Tyler.

Huku akimjibu mwanablogu, mwanamume huyo hata hivyo alidai kuwa shutuma hizo ‘hazina msingi wowote’ na kuongeza kuwa, “Isipokuwa kama ana uthibitisho wowote kwamba nilivujisha picha za uchi.”

Aliendelea kueleza kwamba walikuwa marafiki wa kufaidiana kwa muda mrefu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!