Home » Ringtone afunguka mazito ya Moyoni

Na Burare Kennedy

Mwanamuziki Ringtone Apoko ameamua kutoa ya moyoni, amewachana wadau wa muziki wa injili nchini DJ Moz na Njugush kwa kitendo cha kutowazingitia wasanii wa Gospel kwenye hafla ya mkesha wa mwaka mpya.

Kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Ringtone ameonesha kutofurahishwa na hatua ya wawili hao kumpa kipau mbele rapa King Kaka kwenye hafla hiyo ambayo kwa mujibu wake ilipaswa kuongozwa na wasanii wa nyimbo za injili.

Hitmaker huyo wa “Omba” amesema kitendo cha msanii huyo wa kidunia kulipwa shilling laki mbili kutumbuiza kwenye shoo hiyo ambayo imefadhiliwa na hisani ni njia ya kuivunjia heshima tasnia ya muziki wa injili ikizingatiwa kuwa wasanii wengi wa gospel siku huyo hawakuwa na shughuli ya kufanya.

“Maze nimejam,nimejam , nimejam sana,nimejam can you imagine ati King Kaka aliperform kwa event ya gospel akalipwa 200 thousand shillings na wasanii wa gospel siku hiyo walilala nyumbani hawana pahali pa kwenda kuimba!.,” Alisema kwenye video hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!