Home » Washukiwa Tisa Watoroka Katika Kituo Cha Polisi Cha Isiolo

Washukiwa Tisa Watoroka Katika Kituo Cha Polisi Cha Isiolo

Washukiwa tisa wa uhalifu, miongoni mwao watu wazima na vijana, kwa sasa wanasakwa baada ya kutoroka kutoka Kituo cha Polisi cha Isiolo jana Jumanne.

 

Ripoti zinasema kuwa tisa hao, wote wakiwa na mashtaka ya jinai, walitoroka mwendo wa saa nne asubuhi baada ya kudaiwa kuvunja kufuli ya chumba chao cha mahabusu Kisha walifanikiwa kukimbia kutoka kwa eneo hilo chini ya hali isiyoeleweka.

 

Maafisa wa ulinzi na polisi wanaosimamia dawati la OB inasemekana hawakugundua kuwa tisa hao hawakupatikana hadi saa kadhaa baada ya kutoroka licha ya kwamba seli za ziko karibu na dawati la OB.

 

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Isiolo William Kiambi alisema kwamba polisi wameanzisha msako wa kuwakamata tena washukiwa hao.

 

Aliongeza kuwa kwa sasa polisi wanachunguza jinsi wahalifu hao walivyovunja kufuli kwenye seli zao na kutoroka kusikojulikana licha ya kuwepo kwa walinzi na maafisa wa dawati la OB.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!