Home » Muturi Kupinga Uamuzi Dhidi Ya Uteuzi Makatibu Tawala 50

Muturi Kupinga Uamuzi Dhidi Ya Uteuzi Makatibu Tawala 50

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Justin Muturi amewasilisha ombi la kukata rufaa juu ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa Jumatatu uliobatilisha uteuzi wa Makatibu Wakuu 50 wa Utawala (CASs) wa Rais William Ruto.

 

Kesi hiyo, ambayo imeidhinishwa kuwa ya dharura, itatajwa hii leo Jumatano saa tatu asubuhi mbele ya Jaji Mugure Thande.

 

Katika uamuzi wa Jumatatu, majaji Kanyi Kimondo, Hedwig Ong’udi na Aleem Visram, waliamua kwamba ushiriki wa umma katika uundaji wa nyadhifa za CAS ulifanywa kwa wakazi 23 pekee na uundwaji wa wakazi 27 zaidi haukuzingatia matakwa ya kikatiba ya ushiriki wa umma.

 

Huku ikibainisha kuwa nafasi hiyo ilifutwa mwaka jana, mahakama ilisema; “Mara tu ofisi hiyo ilipofutwa tarehe 21 Septemba 2022, afisi mpya iliyoundwa na wahudumu 23 hawakuweza kufaidika tena.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!